Tuesday, February 12, 2008

KARIBUNI,uliza, sema,tushirikishe, fichua, fundisha

Ndugu nawasalimia katika jina la Yesu Kristo,

Madhumuni ya hii blog ni kufundishana maneno ya Mungu, changamoto mbalimbali tulizonazo, kueleza ukweli wowote bila kuogopa.

Tuna makanisa mengi sana nchini mwetu, lakini pia kuna maovu mengi yanatendeka ndani ya kanisa hilohilo ambalo tulitegemea watu wenye mfano watatoka humo.

Kuwa huru kutoa mawazo yako yoyote juu ya ukristo wetu, nini kinakosewa nini kirekebishwe na wapi tunapata reference kutoka ndani ya biblia.

Naamini muda si mrefu ujao itakuwa ni moja ya website zinakazokuwa za mfano na zinapendwa na watu.Toa mawazo yako usikike. miaka miwili ijayo, litaanzishwa gazeti lenye same title ya blog hii.Ni mahali pa heshima hatutegemei matusi.

Unafanya nini kuujenga ufalme wa Mungu?? mfundishe mwenzako kitu ingawa kidogo, kama unamkosoa kwa lugha ya upole na upendo, kama unafichua maovu taja jina ni wapi na tutawasaidia vipi hao watu.

kama umekata tamaa uliza hapa, utasaidiwa, unashida ya maombi eleza hapa, tutaomba.Unaushuhuda sema hapa tufurahi wote. na zaidi na zaidi ........



Mbarikiwe

Mimi ninaitwa

Imani Kalenge